Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya lampitisha Mheshimiwa Dor Mohamed Issa kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kupigiwa kura 47 za ndiyo kati ya kura 49 zilizopigwa na wajumbe wa Baraza hilo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya ndugu Saitoti Zerothe Stevene amesema kura halali zilizopigwa zilikuwa kura 49 huku kukiwa hakuna kura iliyoharibika na kura za hapana zikiwa ni kura 2 tu.
Wakati huohuo Saitoti amemtangaza Bibi Agnes Mangasila kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kupigiwa kura za ndiyo 46 huku jumla ya wapiga kura wakiwa 49 na kura za hapana zikiwa 3
Akitoa shukrani zake Mheshimiwa Dor aliwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura nyingi huku akiahidi kutoa ushirikiano kwa baraza la Madiwani ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Jiji la Mbeya linapiga hatua za kimaendeleo.
Wakati huohuo Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson wakati akitoa salamu zake amesema kuwa katika kikao kijacho cha Baraza la Madiwani hoja kubwa zikawe vipaumbele vya miradi ya maendeleo ya wananchi na sio kuleta hoja binafsi.
Baraza la Madiwani hilo ni Baraza la kwanza kufanyika tangu uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani kufanyika Octoba 28, 2020.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.