Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wapitisha kiasi cha Shilingi 74,964,752,348/= kama Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mpango wa Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Akiwasilisha makadirio hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bwana Amede E.A, Ng’wanidako amesema Halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha Shilingi 74,964,752,348/= huku fedha hizo zikigawanyika kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo kiasi cha shilingi 16,645,537,804/= ambacho kitakusanywa kutokana na mapato ya ndani, Shilingi 1,642,881,000/= ikiwa ni ruzuku kutoka serikali kuu (OC), shilingi 49,002,520,000/= sehemu ya ruzuku kutoka serikali kuu itakayohusika na mishahara ya watumishi, Shilingi 3,581,811,044/= kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Huku Shilingi 2,892,002,500/= zikiwa ni fedha za Elimu bila Malipo na Shilingi 1,200,000,000/= zikitarajiwa kuwa michango ya wananchi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Aidha Amede amesema katika kipindi cha 2021/2022 Halmashauri imekusudia kutumia jumla ya Shilingi 74,964,752,348/= kati ya hizo , vyanzo vyake vya ndani ni shilingi 16,645,537,804/=, Ruzuku ya mishahara shilingi 49,002,520,000/=, Matumizi ya kawaida Shilingi 1,642,881,000/=, Miradi ya maendeleo ni Shilingi 3,581,811,044/=, Elimu bila malipo Shilingi 2,892,002,500/= huku michango ya wananchi ikikadiriwa kufikia kiasi cha shilingi 1,200,000,000/=
Akiendelea na maelezo yake Mkurugenzi Amede amesema Jiji la Mbeya limekisia kukusanya Shilingi 16,645,537,804/= kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani ya Halmashauri , huku makisio hayo yakiongezeka kutoka Shilingi 15,949,288,000/= kwa mwaka wa fedha 2020/2021, ongezeko hilo linatokana na Mapato yatokanayo na mauzo ya viwanja na makusanyo yatokanayo na Ada za wanafunzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza inayojengwa katiak Kata ya Nsalaga, aidha kiasi cha shilingi 7,304,232,580 sawa na 69.4% ya mapato yasiyolindwa kimetengwa kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa upande wa vipaumbele Halmashauri ya Jiji la Mbeya imepanga kuboresha miundombinu ya Elimu msingi kwa kujenga idadi ya madarasa 52, kutengeneza madawati 900 na matundu ya vyoo 52, kuboresha miundombinu ya Elimu sekondari kwa kujenga madarasa 50, madawati 1,250 na matundu ya vyoo 54, Kujenga vituo vitatu vya afya, Kujenga kitega uchumi cha Hostel ya kupangisha wanafunzi wa vyuo, Kulipa madeni ya wazabuni, Kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuboresha mifumo ya kukusanyia mapato.
Mara baada ya wasilisho hilo la Mkurugenzi ndipo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dormohamed Issa Rahmat alipo wauliza wajumbe kama wanakubaliana na wasilisho hilo la Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya. Wajumbe hao wote kwa pamoja waliafiki Makadirio hayo kuwa mpango wa Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.