MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Akson amewataka Madiwani waliokula kiapo kwenda kuwatumikia wananchi kwa kuwasilisha kero zao kwenye vikao vya Mabaraza na si kuwasilisha mawazo yao binafsi.
Dkt,Tulia ameeleza hayo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kilicho husisha matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuapa kwa Madiwani wote,kura kiapo cha uadilifu na kufanya uchaguzi wa Mstahiki Meya na Naibu Meya wa Jiji la Mbeya kilichofanya katika ukumbi wa Mkapa.
Amesema madiwani hao wanapaswa kuweka hoja za wananchi na sio hoja zao binafsi na kutoa kipaumbele kwa changamoto zinazowakabiri wananchi wa maeneo yao, hivyo wanatakiwa kuleta maendeleo katika Kata zao.
Dkt.Tulia amesema kuwa kila Diwani anatakiwa kujua wajibu wake wa kuwasikiliza wananchi wao ili kuweza kuwaletea maendeleo.
Nae Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe: William Paul Ntika amesema kuwa kwasasa Mbeya inapendeza hivyo Madiwani waliochaguliwa watoe ushirikiano katika suala zima la shughuli za maendeleo la Jiji hilo.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Meya na Naibu Meya Msimamizi wa uchaguzi huo ,Saitot Zelothe Stevene amewatangaza Agnes Mangasila kuwa Naibu Meya wa Jiji la Mbeya kwa kupata kura 46 ,huku Meya wa Jiji la mbeya akitangazwa ndugu DorMohamed Issa ambaye alipata kura 47.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.