Ni maneno ya msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini James Cola Kasusula
Msimamizi huyo pia amewashukuru wananchi,wasimamizi na vyombo vya ulinzi na usalama Jijini humo,kwa kumaliza zoezi la uchaguzi Mdogo wa Madiwani uliofanyika september 16,2018 pasipokua na uvunjifu wa amani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Kasusura amesema tangu kuanza kwa kampeni mpaka siku ya uchaguzi hakujatolewa taarifa yoyote iliyotishia usalama wa raia,licha ya kuwepo kwa ukiukwaji mdogo wa taratibu za uchaguzi kwa chama cha mapinduzi CCM na CHADEMA ambao walipewa barua za onyo mbili kwa CCM na moja kwa CHADEMA.
Amesema ukiukwaji uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi ni kuandamana baada ya kampeni wakijua ni kosa,pamoja na kiongozi mkubwa wa serikali kutumia gari la serikali kwenda kwenye kampeni kitu ambacho siyo sahihi.
Kwa upande wa Chadema,Kasusura amesema nao waliandamana baada ya muda wa kampeni kuisha ambapo waliandikiwa barua moja ya onyo ambayo walikiri kutofanya tena kitendo hicho.
Kuhusu siku ya uchaguzi,September 16 amesema,zoezi lilianza vizuri na kwani vifaa vilifika kwa wakati ikiwemo watendaji na wasimamizi kwenye jumla ya vituo 61 vya kata zote tatu.
Amesema alianza kuzungukia vituoni saa nne asubuhi kuangalia hali ya zoezi, na hapakuwa na malalamiko licha ya baadhi ya Viongozi na wagombea wa CHADEMA kudai kuwa kuna uonevu ikiwemo tukio la kumpiga mgombea wa udiwani ambapo amesema tuhuma hizo hazikuwa na ukweli kwani aliongea na mawakala na baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la tukio ambao walisema uchaguzi unaendelea vizuri.
Hata hivyo Kasusura amewataka viongozi na wanachama wa CHADEMA kukubaliana na matokeo na kuacha propaganda, kwani walitumia mbinu shirikishi ya kuhesabu kura ambapo kila mmoja alijiridhisha na matokeo ya kwenye vituo mpaka yalipotangazwa jumla,na kuongeza kuwa endapo kungekuwa na ubadilishaji wa kura basi mawakala wangegoma kusaini matokeo lakini hakuna wakala aliyegoma kusaini.
Uchaguzi wa madiwani katika Kata tatu za Nsalaga,Maanga na Iwambi ulifanyika september 16 mwaka huu,ambapo CCM ilishinda kwa kishindo dhidi ya CHADEMA katika Kata zote tatu.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.