Halmashauri ya Jiji la Mbeya ipo mbioni kupima ardhi eneo la Mwansekwa ambalo lipo pembezoni mwa Jiji hilo, Kata ya Mwansekwa ni miongoni mwa Kata 36 zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Akiwasilisha mpango wa Jiji hilo mbele ya wananchi wa Mwansekwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bwana Amede E.A, Ng’wanidako amewaeleza wananchi hao kuwa dhana ya mabadiliko ni ya lazima na kwakuwa Mji unakuwa hivyo wananchi hao hawana budi kukubaliana na mpango wa serikali wa kupima maeneo yao ili kuipa thamani ardhi yao na kuufanya mji wa Mbeya kupangika katika ramani ya nchi.
“Ndugu zangu kama ilivyo kwa mwanadamu huzaliwa kisha hukua na kufariki kadhalika na kwenye maisha yetu inatupasa kuwa hivyo kwa maana ya kubadilika na kuendana na hali halisi ya sasa” Alisema Mkurugenzi Amede
Aidha Mkurugenzi Amede aliwaeleza wananchi hao kuwa hatua hiyo ni ya awali ya kuwashirikisha wananchi wote ili wapate uelewa wa nini serikali imepanga kutekeleza katika eneo hilo.
Wananchi wa Kata hiyo walionyesha hofu kubwa ya endapo eneo hilo litapimwa nini itakuwa hatma yao katika maeneo hayo, Bibi Jenipher Mwamboneke mkazi wa Mwansekwa alieleza kuwa kama Jiji litapima viwanja hivyo watapata wapi maeneo ya kulima na kuendesha maisha yao.
Akijibu hoja za wananchi hao Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Wilam Paul Ntinika amewatoa hofu wananchi hao na kuwaahidi kuwa kila mwenye haki atapata haki yake huku akiielekeza Halmashauri katika zoezi hilo la upimaji kutoa kipaumbele kwa wamiliki wa ardhi wa asili
“ Ngugu zangu msiwe na hofu yoyote serikali ipo hapa kwaajili yenu hakuna atakaye nyimwa haki yake, kila mwenye haki atapata stahiki zake” aliongezea DC Ntinika
DC Ntinika ameutaka uongozi wa Kata hiyo kukaa na wananchi hao ili kutoa elimu zaidi huku akimtaka Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Juma Changani kutembea ikiwezekana nyumba kwa nyumba kwa kila mwananchi ili kila mwananchi apate uelewa wa nini serikali imepanga kufanya katika eneo hilo.
Eneo la Mwansekwa limelengwa kupimwa na Jiji la Mbeya kutokana na jinsi mji unavyokuwa siku hadi siku huku inakadiriwa kuwa na ongezeko la idadi ya watu katika Jiji la Mbeya ambalo linapelekea uhitaji mkubwa wa ardhi kwa matumizi mbalimbal
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.