Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeadhimisha siku ya Wanawake Dunia kwa kutangaza kupambana na unyanyasaji wa kijinsia kwa watumishi ambao watakwenda kinyume na haki za mwanamke na binadamu kiujumla.
Akiongea kwenye hafla ya maadhimisho hayo yaliofanyika kwenye ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi.Agnes Mangasila amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake na kuwataka wanawake watumishi wasimuangushe, watende kazi ipasavyo kama ambavyo mkuu huyo wa nchi anavyopambana kuleta maendeleo.
Aidha Naibu Meya Mangasila amefafanua kuwa Mkoa na Jiji la Mbeya limekuwa na bahati mwaka huu kwa kumpata kiongozi mkuu wa moja ya mihili mitatu ya nchi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Tulia Ackson ambaye ni mwanamke mpigania maendeleo bila kujali yanakwenda upande gani wa nchi hivyo amewataka wanawake waendelee kuamka kupambania haki na maendeleo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji Bi.Upendo Haule ambaye pia ni Mkuu wa idara ya Utawala na Utumishi amesema hatakuwa tayari kuona unafanyika unyanyasaji wowote wa kijinsia kwenye Halmashauri Jiji la Mbeya ambayo yeye anaisimamia katika sekta ya utumishi na utawala .
Bi. Upendo Haule amewataka wale wote watakaopatwa na kadhia ya unyanyasaji wa kijinsia wasisite kutoa taarifa ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wanaofanya tabia hiyo inayopingwa Duniani na mbinguni.
“Mimi ndiye ninayesimamia nidhamu ya watumishi naomba mwanamke yeyote ambaye atafanyiwa kitendo cha unyanyasaji kazini atoe taarifa kwenye ofisi yangu hakuna atakayesalimika kwa mujibu wa sheria “amesema Bi.Upendo Haule Mkuu wa idara ya Utawala na Utumishi wa Jiji la Mbeya.
Sherehe ya siku ya Wanawake hufanyika Duniani kote kila mwaka ifikapo Machi 8 ambapo kwa Tanzania mwaka huu kitaifa imefanyika Unguja Visiwani Zanzibar huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan zikiwa na kauli mbiu Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu .
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.