Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi 605,000,000/= kwa vikundi vya wajasiriamali 31 vikiwemo vikundi vya wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu kwa robo ya nne ya mwaka 2021/2022.
Mikopo hiyo imetolewa kwa vikundi 31 vilivyopo Jiji la Mbeya na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini mheshimiwa Dkt: Tulia Ackson.
Akimkaribisha Spika kukabidhi hundi ya mkopo huo Mstahiki meya wa Jiji la Mbeya mheshimiwa Dormohamed I Rahmat ameelezea namna Halmashauri ya Jiji la Mbeya inavyotekeleza kwa vitendo maelekezo na miongozo ya serikali kwa kutoa mikopo hiyo kwa mujibu wa sera na miongozo ya nchi.
Nae Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Wakili Triphonia Kisiga amemshukuru Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo anayoifanyia nchi kwani mikopo hii hutolewa bila riba kwa wakopaji.
Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia 2021/2022 imeshatoa kiasi cha Bilioni 1.7 kwa makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.