• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbeya City Council
Mbeya City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Health,Social Welfare and Nutrition services Division
      • Agriculture,Livestock and Fisheries Division
      • Human Resources Management and Administration Division
      • Pre Primary and Primary Education Division
      • Secondary Education Divison
      • Infrastructure,Rular and Urban Development Division
      • Planning and Coordination Division
      • Industry, Trade and Investments Division
      • Community Development Division
    • Vitengo
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • ICT Unit
      • Legal Services Unit
      • Finance and Accounts Unit
      • Government Communication Unit
      • Natural resources and Environment Conservation
      • Sports, Culture and Arts Unit
      • Ward Executive Office
      • Village/Mtaa Executive Office
      • Waste Management and Sanitation
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
    • Orodha ya Wah Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

Imewekwa Tarehe: July 31st, 2024

Mbunge wa Mbeya Mjini, Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Mabunge Duniani Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema imefika wakati sasa jiji la Mbeya kuanza kupima ardhi kwa ajili ya uwekezaji badala ya kuendelea kupima viwanja kwa ajili ya makazi lengo likiwa ni kuongeza mapato yatakayotokana na huduma za kijamii.

Mhe. Mbunge ametoa wito huo leo tarehe 31 Julai, 2024 wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani  kilichofanyika katika Ukumbi wa Mstahiki Meya uliopo kwenye jengo la  Halmashauri ya Jiji la Mbeya chini ya Mstahiki Meya  wa Jiji Mhe. Dor Mohamed Isssa.

Dkt. Tulia amesema Jiji la Mbeya linatakiwa kubadilika kwa kuweka maeneo ya uwekezaji ambayo yatawezesha kutoa huduma za kijamii kama vile  mahoteli makubwa, kumbi  kubwa za kisasa za mikutano ambazo zitaongeza  mapato ya Jiji.

Amesema kwa sasa Jiji na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla hauna ukumbi unaoweza kubeba zaidi ya watu 5,000 hivyo kuwa vigumu hata kwa mikutano ya kimataifa kufanyika katika jiji la Mbeya, hivyo ni wakati muafaka kuwekeza katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za ghorofa  kwa ajili ya makazi na biashara.

"Tunashukuru uwanja wa Ndege wa Mbeya umekamilika na ndege za aina yoyote zinaweza kutua , changamoto iliyopo  ni ukosefu wa hoteli kubwa (Five Star Hotels) jambo linalosababisha ndege za kimataifa kutotua uwanja wa Mbeya," amefafanua Dkt. Tulia.

Dkt. Tulia amewapongeza Madiwani chini ya uongozi wa Mstahiki Meya pamoja na watendaji wa Halmashauri kutokana na utekelezaji wa majukumu bambalimbali katika kipindi cha mwaka 2023/2024 ambapo wameweza kusimamia vizuri miradi ya maendeleo na usafi wa mazingira na kuliwezesha Jiji kushika nafasi ya pili kwa usafi.

Amesema katika mwaka wa Fedha 2023/2024 suala la elimu lilipewa kipaumbele na kuwezesha ujenzi wa matundu ya vyoo , ujenzi wa madarasa, ukarabati wa majengo ya shule zote za msingi na ununuzi wa madawati mpango ukiwa ni kuziweka  shule zote katika hadhi inayotakiwa na  kuwa mfano wa kuigwa  na Halmashauri nyingine Tanzania.

"Tumejenga matundu 350 ya vyoo mashuleni, kwa mwaka huu wa fedha  matundu 156 ya vyoo yatajengwa na kufanya pungufu ya matundu ya vyoo kuwa 60," amefafanua Dkt. Tulia.

Aidha Mheshimiwa Dkt. Tulia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

Mstahiki Meya kwa upande wake amemshukuru Dkt. Tulia kwa jitihada anazofanya kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo jijini Mbeya anafanyika kwani katika mwaka wa fedha 2023/2024  kiasi cha shilingi Bilioni 38.7 zilitolewa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuhimiza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa madiwani wanapewa taarifa  pindi fedha za miradi zinapopelekwa katika maeneo yao ili wasimamie kwa ukamilifu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw. John Nchimbi amesema kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 Halmashauri imetenga kiasi cha Shilingi milioni 871 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo na ukarabati  wa shule zenye changamoto.

Mwisho

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AJIRA YA MKATABA KWA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO ( ORAL III C) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO (ORAL III B) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO(ORAL III A) April 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MOTISHA ZATOLEWA KWA WALIMU WAKUU KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI

    January 24, 2025
  • WAANDIKISHAJI WA UCHAGUZI WAAPISHWA JIJINI MBEYA

    October 08, 2024
  • JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

    July 31, 2024
  • JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

    July 31, 2024
  • Tazama Zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

"MSITUBIPU KATIKA UCHAGUZI " RC MBEYA
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mbeya City Football Club
  • Google
  • Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu

Tovuti Mashughuli

  • Poralg Website
  • Ikulu Website
  • Public Service Website
  • Tanzania Website
  • eGA
  • Secretariati ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Mbalizi Road near TTCL Offices

    Anuani ya Posta: 149 Mbeya

    Simu: +25525252502372

    Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563

    Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.