• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbeya City Council
Mbeya City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Health,Social Welfare and Nutrition services Division
      • Agriculture,Livestock and Fisheries Division
      • Human Resources Management and Administration Division
      • Pre Primary and Primary Education Division
      • Secondary Education Divison
      • Infrastructure,Rular and Urban Development Division
      • Planning and Coordination Division
      • Industry, Trade and Investments Division
      • Community Development Division
    • Vitengo
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • ICT Unit
      • Legal Services Unit
      • Finance and Accounts Unit
      • Government Communication Unit
      • Natural resources and Environment Conservation
      • Sports, Culture and Arts Unit
      • Ward Executive Office
      • Village/Mtaa Executive Office
      • Waste Management and Sanitation
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
    • Orodha ya Wah Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

MADIWANI JIJI LA MWANZA W APATIWA MBINU ZA UBORESHAJI MAPATO

Imewekwa Tarehe: March 23rd, 2024

Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza limefanya ziara ya siku moja katika Jiji la Mbeya ili kujifunza namna ya kuboresha shule za msingi za mchepuo wa kiingereza na uwekezaji wa pamoja kati ya Serikali na wabia binafsi kwa lengo la kuboresha mapato ya Halmashauri.

Akizungumza wakati wa kutembelea miradi ya Shule za Msingi za mchepuo wa kiingereza na uwekezaji wa eneo la burudani na starehe(City Park) Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe.Sima Costantine amesema hii ni mara ya pili kufanya ziara katika Jiji la Mbeya, kwani walifanya hivyo miaka mitano iliyopita kipindi ambacho kulikuwa na shule moja ya msingi ya mchepuo wa kiingereza na baada ya ziara hiyo  walifanikiwa kujenga shule moja ya mchepuo wa kiingereza ambayo imekuwa moja ya vyanzo  muhimu vya mapato jijini Mwanza.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ameongeza kuwa wanahitaji kuongeza idadi ya shule biashara za mchepuo wa kiingereza, hivyo wameona warudi kujifunza tena Jiji la Mbeya ambalo kwa sasa linamiliki shule tano(5) za mchepuo wa kiingereza na kulifanya Jiji la Mbeya kuwa  la mfano kwa halmashauri nyingine nchini.

“Jiji la Mbeya limefanya mapinduzi makubwa ya kiundeshaji hasa kwenye sekta hii ya elimu ya shule za mchepuo wa kiingereza lengo letu ni kuongeza idadi ya shule katika Jiji la Mwanza tumerudi tena kwa mwalimu wetu aliyetupatia mbinu za kuanzisha mradi ambao umekuwa mkubwa katika kuliingizia mapato jiji letu,”amesema Mhe. Costantine.

Aidha Mstahiki Meya huyo wa Jiji la Mwanza ameongeza kuwa Jiji hilo lina maeneo ya kutosha hivyo wamevutiwa na kuona kuna kila sababu ya kuja kujifunza juu ya uwekezaji wa pamoja kati ya Serikali na wabia binafsi kama Jiji la Mbeya linavyofanya katika uwekezaji wa mradi wa kituo cha burudani na starehe, maarufu City Park utakaogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni Nne za kitanzania mpaka kukamilika kwake.

Mhe. Constatine ameupongeza mkataba kati ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya na muwekezaji ambao una muda maalum wa kiuendeshaji kwa muwekezaji baada ya hapo  unakuwa chini ya miliki ya Halmashauri na kupangiwa utaratibu mwingine wa kiundeshaji kadri itakavyohitajika.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amesema ziara ya madiwani na watendaji wa  Jiji la Mwanza inaendelea kuwatia shime katika kubuni na kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa chachu kwa halmashari nyingine nchini kuja kujifunza.

Jiji la Mbeya kwa sasa linamiliki shule tano (5) za msingi za mchepuo wa Kiingereza ambazo ni Chief Rockert Mwashinga, (Kata ya Nsalaga), Magufuli (Kata ya Iyela), Mkapa (Kata ya Ruanda) na Azimio pamoja na Umoja(Kata ya Sisimba).  

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AJIRA YA MKATABA KWA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO ( ORAL III C) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO (ORAL III B) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO(ORAL III A) April 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MOTISHA ZATOLEWA KWA WALIMU WAKUU KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI

    January 24, 2025
  • WAANDIKISHAJI WA UCHAGUZI WAAPISHWA JIJINI MBEYA

    October 08, 2024
  • JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

    July 31, 2024
  • JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

    July 31, 2024
  • Tazama Zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

"MSITUBIPU KATIKA UCHAGUZI " RC MBEYA
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mbeya City Football Club
  • Google
  • Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu

Tovuti Mashughuli

  • Poralg Website
  • Ikulu Website
  • Public Service Website
  • Tanzania Website
  • eGA
  • Secretariati ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Mbalizi Road near TTCL Offices

    Anuani ya Posta: 149 Mbeya

    Simu: +25525252502372

    Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563

    Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.