Wananchi Halmashauri ya Jiji la Mbeya wametakiwa kujitokeza kwenye zoezi la chanjo ya Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko19 linaloendelea katika vituo mbalimbali baada ya kuzinduliwa hivi karibuni Ikulu jijini Dar es salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dormohamed Issa ametoa wito huo alipokuwa akishiriki kwenye zoezi la chanjo lilofanyika kwenye Kituo cha Afya Kiwanja Mpaka na amewatoa hofu wananchi kuwa wataalam wamethibitisha kuwa Chanjo hiyo haina madhara hivyo wananchi wajitokeze kwa hiyari kupata chanjo kwa vile bado ugonjwa huo unaitikisa Dunia na kusababisha vifo vingi.
Aidha Meya huyo amendelea kuwafafanulia wakazi wa Jiji la Mbeya kuwa hata miaka ya nyuma zilipokuja chanjo za magonjwa mbalimbali yalikuwa yakizushwa maneno mengi lakini yeye na watu wenye umri kama wake walichanja na hakuna madhaara yaliyojitokeza hivyo amewataka kuacha kusikiliza maneno yasiyo na msingi kwenye afya bali kufuata maelekezo na kuzingatia taarifa na tahadhari zitolewazo na wataalamu.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt.Jonas Lulandala amewataka wananchini kutokuwa na hofu juu ya Chanjo hiyo ya Uviko19 (Covid19) ambayo ni muhimu kuchanja kwa vile janga hili limesumbua ulimwengu mzima ambao mpaka sasa uko kwenye mapambano hivyo asiyechanja atakuwa anajitenga na ulimwengu.
Mganga mkuu huyo wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ameongeza kuwa umuhimu wa chanjo ni kuzuia kupata ugonjwa wa Uviko19 na hata ukiupata haukuletei athari na madhara makubwa kama yule asiye Chanja.
Aidha Dkt.Lulandala amefafanua kuwa awali katika Halmashauri ya jiji la Mbeya kuliwa na vituo vitatu vya Chanjo ambavyo ni Hospitali ya rufaa Kanda, Hospitali ya rufaa Mkoa na Hospitali ya Igawilo lakini baada ya kuona uhitaji na umuhimu wa zoezi la Chanjo wameongeza kituo kimoja ambacho ni Kituo cha afya Kiwanja Mpaka na kufikia vituo vinne vya kutolea ya chanjo Uviko19 kwasasa.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.