Wakuu wa Wilaya zote Mkoani Mbeya wametakiwa kuanzisha Kampeni za usafi na kutunza mazingira ili kuufanya Mkoa huo uwe na wakazi wenye afya wanaoishi katika mazingira mazuri ambayo yanaweza kuwavutia wawekezaji kwenye sekta mbalimbali zilizopo Mkoa Mbeya.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Juma Zuberi Homera alipokuwa akizindua kampeni ya “WEKA JIJI SAFI” hafla iliyofanyika katika Stand ya daladala ya Kabwe ambapo ametaka Wakuu wa Wilaya za Chunya ,Rungwe , Mbarali na Kyela kuiga mfano kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya iliyondani ya Wilaya ya Mbeya.
Aidha Mh.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka viongozi hao kwenda kuzisimamia ipasavyo sheria ndogo ndogo ambazo Halmashauri zimekasimishwa na Bunge kuzitunga ikiwemo faini za uharibifu na uchafuzi wa mazingira ambazo zinalinda na kutunza madhari ya Mkoa wa Mbeya na Halmashauri zake.
Katika uzinduzi huo baadhi ya wafanyabiashara katika masoko wakiwemo wafanyabiashara wa Soko la Soweto Jijini Mbeya wameonesha kuunga mkono kampeni ya WEKA JIJI SAFI kwa kufika kwenye uzinduzi huo na bango lenye ujumbe SOKO LA SOWETO BILA UCHAFU LINAWEZEKANA.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt.Tulia Ackson amewaomba wakazi wa Jimbo lake kutunza mazingira ili kuendelea kuivutia Serikali kuijenga Mbeya kama ambavyo imeahidi likiwemo suala la ujenzi wa barabara nne kutoka Uyole mpaka Mbalizi na ujenzi wa Hospitali na miundombinu ya elimu inayoendelea kujengwa kwenye jiji la Mbeya na Mkoa wa Mbeya kiujumla.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.