• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbeya City Council
Mbeya City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Health,Social Welfare and Nutrition services Division
      • Agriculture,Livestock and Fisheries Division
      • Human Resources Management and Administration Division
      • Pre Primary and Primary Education Division
      • Secondary Education Divison
      • Infrastructure,Rular and Urban Development Division
      • Planning and Coordination Division
      • Industry, Trade and Investments Division
      • Community Development Division
    • Vitengo
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • ICT Unit
      • Legal Services Unit
      • Finance and Accounts Unit
      • Government Communication Unit
      • Natural resources and Environment Conservation
      • Sports, Culture and Arts Unit
      • Ward Executive Office
      • Village/Mtaa Executive Office
      • Waste Management and Sanitation
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
    • Orodha ya Wah Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

VYAMA VYA SIASA VYARIDHISHWA USHIRIKISHWAJI MABORESHO YA MPANGO MKAKATI WA JIJI LA MBEYA

Imewekwa Tarehe: May 31st, 2024

Vyama vya siasa Wilayani Mbeya kwa pamoja vimeafiki namna ambavyo mchakato wa maboresho ya Mpango Mkakati wa miaka mitano(2024/25 - 2029/30) wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya unavyofanyiwa kazi kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

 Akizungumza kwenye kikao  cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Mbeya(DCC) Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mbeya Mjini Bw.Persi Mapunda amesema kilichofanywa na Serikali ya Wilaya ni jambo muhimu kwa kuwashirikisha kwasababu wao ndio wanaowawakilisha wananchi kupitia vyama vyao wanavyoviongoza.

Katibu huyo wa Chadema ameongeza kuwa watumishi na  wapiga kura wao ndio wenye Mbeya hivyo ushirikishwaji ni lazima na muhimu kama kamati ya ushauri ya Wilaya ilivyofanya ili kupata maoni na kufikia malengo ya kuboresha Mpango Mkakati wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Kwa upande wake katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mbeya Mjini, Bw.Ibrahim Mwamkwama amesema, wameridhishwa na  ushirikishwaji katika kuhakikisha  Mbeya ijayo inakuwa bora kwa mwananchi mmoja mmoja na jamii kwa ujumla, hasa  kwa kuboresha mpango wa mikopo ya asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji, inayoelekezwa kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Naye katibu wa chama cha ACT-Wazalendo Mbeya Mjini, Bw.Gift Almas amepongeza uendeshwaji wa zoezi la maboresho la mpango Mkakati tangu kuanza kwake kwa kuwashirikisha wananchi,viongozi wa kimila, wafanyabiasha, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa, kwa kufanya hivyo Kamati ya Ushauri ya Wilaya imezingatia mambo muhimu kuelekea kuipata Mbeya yenye kukua na kuendelea kiuchumi, kisiasa na nyanja nyingine muhimu za kimaendeleo.

Pamoja na hayo Katibu huyo wa ACT-Wazalendo amewaasa wakazi wa Jiji la Mbeya na Wilaya kwa ujumla kujitokeza kwa wingi wakati litakapoanza zoezi la kuboresha Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili kujiweka tayari kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.

Akimwakilisha Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Mbeya ,Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amewapongeza wadau kwa kushiriki vyema kikao hicho na kuwahimiza kuendelea kuwasilisha maoni yao kwa kamati husika ili  kuijenga Mbeya kwa pamoja.

Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Mbeya(DCC) inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe.Beno Malisa inaendelea kukusanya maoni ya wadau mbalimbali ili kukamilisha maboresho ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Halmshauri ya Jiji la Mbeya. Unaotarajiwa kuanza kutekelezwa ifikapo Julai 2024.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AJIRA YA MKATABA KWA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO ( ORAL III C) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO (ORAL III B) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO(ORAL III A) April 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MOTISHA ZATOLEWA KWA WALIMU WAKUU KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI

    January 24, 2025
  • WAANDIKISHAJI WA UCHAGUZI WAAPISHWA JIJINI MBEYA

    October 08, 2024
  • JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

    July 31, 2024
  • JIJI MBEYA LATAKIWA KUPIMA ARDHI KWA AJILI YA UWEKEZAJI

    July 31, 2024
  • Tazama Zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

"MSITUBIPU KATIKA UCHAGUZI " RC MBEYA
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mbeya City Football Club
  • Google
  • Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu

Tovuti Mashughuli

  • Poralg Website
  • Ikulu Website
  • Public Service Website
  • Tanzania Website
  • eGA
  • Secretariati ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Mbalizi Road near TTCL Offices

    Anuani ya Posta: 149 Mbeya

    Simu: +25525252502372

    Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563

    Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.