• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbeya City Council
Mbeya City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Health,Social Welfare and Nutrition services Division
      • Agriculture,Livestock and Fisheries Division
      • Human Resources Management and Administration Division
      • Pre Primary and Primary Education Division
      • Secondary Education Divison
      • Infrastructure,Rular and Urban Development Division
      • Planning and Coordination Division
      • Industry, Trade and Investments Division
      • Community Development Division
    • Vitengo
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • ICT Unit
      • Legal Services Unit
      • Finance and Accounts Unit
      • Government Communication Unit
      • Natural resources and Environment Conservation
      • Sports, Culture and Arts Unit
      • Ward Executive Office
      • Village/Mtaa Executive Office
      • Waste Management and Sanitation
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
    • Orodha ya Wah Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

WADAU NA DSW WAKUTANA KUJADILI UIMARISHAJI MIFUMO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

Imewekwa Tarehe: April 24th, 2024

WAKUTANA KUJADILI UIMARISHAJI MIFUMO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA 

Shirika lisilo la kiserikali la DSW Tanzania linalojishughulisha na afya na maendeleo ya vijana kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wametoa mafunzo ya kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia mkoani Mbeya.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa katika kikao kazi kinachofanyika kwenye ukumbi wa Meya  uliopo jengo la Halmashauri ya Jiji la Mbeya tarehe 24-25 Aprili,2024.

 Mkurugenzi wa shirika la DSW Tanzania Bw. Peter Luwaga amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili kwenye nyanja zote kwa watoto na vijana na kujadiliana kuhusu suala zima la ukatili, ulinzi na usalama wa watoto  mtandaoni, ndani na nje ya shule.

Bw.Luwaga amesema kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili kwa vijana  ambao ni kundi kubwa itawawezesha kuendesha uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa na kuepukana na changamoto nyingi zinazosababishwa na mambo mengi  ambayo ni pamoja na changamoto za ajira, afya hivyo stadi za maisha  ni muhimu ili kuepuka na kujiepusha  na vitendo viovu kama madawa ya kulevya.

Kwa upande wake Afisa  Maendeleo ya Jamii Mwandamizi  kutoka Wizara ya Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw.Victor Rugalabamu amesema miongoni mwa sababu  zinazochangia ukatili ni pamoja na mila na desturi potofu,  malezi duni, migogoro katika familia, umaskini wa kipato na imani za kishirikina.

Aidha Afisa mwandamizi huyo ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Watoto  Duniani ( Unicef) mwaka 2015,  Asilimia  Sitini (60%) ya ukatili ulikuwa unafanyika majumbani, hivyo Serikali na Shirika la DSW Tanzania likaanzisha dawati la mifumo ya ulinzi na usalama kwa watoto dhidi ya vitendo vya ukatili.

 Ameongeza kuwa mifumo hiyo  itasaidia kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ukatili kwa vijana na watoto.

 Kwa upande  wake Afisa Elimu Sekondari, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Bi.Matilda Luvanda ameeleza kuwa kuimarishwa kwa mifumo hiyo kutasaidia zoezi la utoaji taarifa kwa wanafunzi wahanga wa matukio ya ukatili yanayofanyika shuleni na majumbani.

Katika kikao hicho shirika la DSW Tanzania limetoa vifaa vya michezo kwenye baadhi ya shule ambavyo ni jezi na mipira sambamba na runinga zitakazokuwa zikitumika kufundishia mapambano dhidi ya ukatili.

Naye mwanafunzi Hance Raymond Mveka amewashukuru wawezeshaji wa shirika la DSW Tanzania kwa vifaa hivyo ambapo runinga zitatumika  kujifunza mbinu za kupambana na ukatili huku akieleza kuwa vifaa vya michezo vitawasaidia kuimarisha vipaji vyao vitakavyowawezesha kupata ajira na kujiongezea kipato.

Kikao kazi hicho kinachofanyika mkoani Mbeya kinahudhuriwa na  Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Elimu Sekondari, Waendesha Mashitaka, Wawakilishi wa Mahakama, Wasimamizi wa Masuala ya Ulinzi na Usalama, Wawakilishi wa Dawati la Jinsia na Wakuu wa Shule katika Halmashauri tatu za  wilaya za Rungwe, Mbeya na Jiji na baadhi ya wanafunzi ambao ni walengwa wakuu. Mikoa mingine itakayonufaika na mpango huu ni pamoja na Songwe, Kilimanjaro na Arusha.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AJIRA YA MKATABA KWA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO ( ORAL III C) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO (ORAL III B) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO(ORAL III A) April 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC.DKT.HOMERA AIPONGEZA JIJI LA MBEYA KWA ONGEZEKO LA MAPATO NA KUPATA HATI SAFI NDANI YA MIAKA MITANO

    June 16, 2025
  • HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI 2025/2030

    June 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI JIJI LA MBEYA LAJIVUNIA MIAKA 5 YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    June 06, 2025
  • MAONESHO YA MBEYA CITY EXPO FURSA KWA WAFANYABIASHARA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

"MSITUBIPU KATIKA UCHAGUZI " RC MBEYA
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mbeya City Football Club
  • Google
  • Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu

Tovuti Mashughuli

  • Poralg Website
  • Ikulu Website
  • Public Service Website
  • Tanzania Website
  • eGA
  • Secretariati ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Mbalizi Road near TTCL Offices

    Anuani ya Posta: 149 Mbeya

    Simu: +25525252502372

    Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563

    Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.