MKUU WA MKOA WA MBEYA MHE;JUMA ZUBERI HOMERA ANAPENDA KUWAJULISHA WAKAZI WA MKOA WA MBEYA KUWA KUTAKUA NA UVUMBUZI WA KUIBUA VIPAJI VYA MPIRA WA MIGUU {MBEYA SUPER CUP 2021 }. KWA VIJANA WENYE UMRI UNAOZIDI MIAKA 23, WANAOTOKA KATIKA HALMASHAURI ZA MBEYA MJINI ,BUSOKELO,CHUNYA, KYELA, MBARALI, MBEYA VIJIJINI NA RUNGWE. KILA HALMASHAURI ITATAKIWA KUTOA TIMU MOJA ISIPOKUA HALMASHAURI YA MBEYA MJINI AMBAYO ITATOA TIMU MBILI. MASHINDANO HAYO YATAFANYIKA UWANJA WA SOKOINE KUANZIA TAREHE.19-8 HADI 25-8 2021 MUDA SAA 4 ASUBUHI
DHUMUNI LA MASHINDANO HAYA NI KUTAFUTA VIJANA WENYE UWEZO WATAKAO JIUNGA NA TIMU ZA MKOA KAMA MBEYA CITY , PRISON NA MBEYA KWANZA.
TIMU ZOTE ZITATAKIWA KUWASILI SIKU YA JUMATANO TAR.18-8-2021 JIONI. KWA KUWASHIRIKISHA VIONGOZI WOTE WA HALMASHAURI MNAOMBWA KUZIWEZESHA TIMU ZENU KWA USAFIRI, VIFAA, MAJI NA TIBA WAKATI WA MASHINDANO. ZAWADI ZITATOLEWA KWA WASHINDI WAFUATAO; ZAWADI MSHINDI WA KWANZA NI KOMBE NA FEDHA, MSHINDI WA PILI NA WATATU WATAPEWA FEDHA TASLIMU.ZAWADI ZINGINE ZITATOLEWA KWA WASHINDI WAFUATAO;
CHAKULA NA MALAZI ZITATOLEWA KWA WASHIRIKI WOTE BURE
SIKU YA UZINDUZI MGENI RASMI ATAKUA NI WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHE; INNOCENT BASHUNGWA .
HAKUNA KIINGILIO NYOTE MNAKARIBISHWA.
Mbalizi Road near TTCL Offices
Anuani ya Posta: 149 Mbeya
Simu: +25525252502372
Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563
Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz
Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.