• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbeya City Council
Mbeya City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Health,Social Welfare and Nutrition services Division
      • Agriculture,Livestock and Fisheries Division
      • Human Resources Management and Administration Division
      • Pre Primary and Primary Education Division
      • Secondary Education Divison
      • Infrastructure,Rular and Urban Development Division
      • Planning and Coordination Division
      • Industry, Trade and Investments Division
      • Community Development Division
    • Vitengo
      • Internal Audit Unit
      • Procurement Management Unit
      • ICT Unit
      • Legal Services Unit
      • Finance and Accounts Unit
      • Government Communication Unit
      • Natural resources and Environment Conservation
      • Sports, Culture and Arts Unit
      • Ward Executive Office
      • Village/Mtaa Executive Office
      • Waste Management and Sanitation
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wah Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
    • Orodha ya Wah Madiwani
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

BARAZA LA MADIWANI JIJI LA MBEYA LAJIVUNIA MIAKA 5 YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Imewekwa Tarehe: June 6th, 2025

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya linalotarajia kumaliza kipindi chake hivi karibuni limeendelea kujivunia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi tangu lilipoingia madarakani baada ya uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amesema tangu walipoingia madarakani kipindi hiki cha awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan miradi mingi ya maendeleo ambayo imetekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija kwa wakazi wa Jiji la Mbeya, Mkoa wa Mbeya na nchi kiujumla.

Miradi ambayo imejengwa katika awamu hii na kuwafanya madiwani wa baraza hilo kujivunia imetekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani na fedha kutoka serikali kuu imegusa miradi ya Afya,Elimu,Barabara na miundombinu yake,Maendeleo ya Jamii kwa kutoa mikopo ya asilimia kumi (10%) kwa Vijana,Wanawake na Watu wenye Ulemavu.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amefafanua kuwa pamoja na miradi mingine ya afya katika hospitali ya Wilaya Igawilo fedha za serikali kuu zimetekeleza mradi wa Ujenzi wa Jengo la dharura (EMD) wenye thamani ya shilingi milioni mia nne(400,000,000) ,mradi wa Ujenzi wa wodi ya upasuaji wanawake wenye thamani ya shilingini milioni mia mbili(200,000,000) na mradi mwingine katika hospitali hii yenye hadhi ya Wilaya ni ujenzi wa wodi ya wanaume ambao una thamani ya shilingi milioni mia mbili(200,000,000) na zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetumika kujenga vituo vya afya kwenye Kata za Isyesye,Itagano,Iyela na Mwakibete awali wananchi wa Kata hizo walikuwa wakitembea umbali mrefu katika kufuata huduma.

Kwa upande wa elimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na laki tisa kupitia mradi wa BOOST zimetumika kujenga shule mpya ya mkondo mmoja yenye madarasa matatu (03) ya mfano ya Elimu ya Awali katika shule ya msingi Iwambi mradi huu una thamani ya shilingi milioni mia tatu Hamsini na laki tano(350,500,000.00), vyumba 9 vya madarasa,Ujenzi wa matundu 6 ya choo  kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya Awali matundu 16 ya vyoo vya wanafunzi wengine na jengo la utawala pamoja na ujenzi wa shule mpya ya mkondo mmoja yenye madarasa  2 ya mfano katika shule ya msingi Mwasanga mradi huu una thamani ya shilingini milioni mia tatu hamsini na laki tano (350,500,000.00),vyumba 9 vya madarasa,ujenzi wa matundu 6 ya choo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya Awali na matundu 16 ya vyoo vya wanafunzi wengine na jengo la utawala.

Aidha Mstahiki Meya amesema Pamoja na miradi hiyo pia fedha za BOOST zimewezesha miradi mingine ya ujenzi wa madarasa na matundu 04 ya vyoo katika shule msingi Mafanikio iliyopo Kata ya Itezi kwa vyumba vya madarasa 3 na ujenzi wa vyoo matundu 6 ukiwa na thamani ya shilingi milioni themanini na nane(88,000,000) na Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na choo cha matundu 6 katika shule ya msingi Igale iliyopo Kata ya Iyunga na mradi mwingine unaotokana na fedha za BOOST ni ujenzi wa vyumba 04 vya madarasa na matundu 06 ya vyoo katika shule ya msingi Tambukareli iliyopo Kata ya Itezi ukiwa na thamani shilingi Milioni mia moja kumi na tatu (113,000,000)

Kwa pamoja Miradi hii ya BOOST yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni mia tisa na laki tisa (990,000,000) inatarajia kupunguza adha ya msongamano wa wanafunzi madarasni,kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu na utawezesha wazazi na walezi kwenye Kata husika na Kata za jirani kufuatilia maendeleo ya Watoto kwa ukaribu.

Aidha Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetumia kiasi cha shilingi milioni 357.939,000 fedha za mapato ya ndani kwa upande wa elimu sekondari shilingi milioni mia mbili arobaini na tatu laki tisa thelethini na tisa elfu (243,939,000) zimetumika katika  kuchangia ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya wasichana Dkt.Tulia(Dr.Tulia Girls' ), kiasi cha shilingi milioni Hamsini na tano(55,000,000) zimetumika katika kukamilisha ujenzi wa maabara 02 katika shule ya Sekondari Dr.Tulia Ackson,kwa upande mwingine kiasi cha shilingi milioni arobaini na tano(45,000,000)zimetumika katika mradi wa kukamilisha ujenzi wa madarasa 03 katika shule ya sekondari ya Itagano na mradi wa mwisho uliotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ni Ujenzi wa vyoo matundu 8 shule ya sekondari Hayombo ukiwa na thamani ya shilingi milioni kumi na nne (14,000,000).

 

Mstahiki Meya amefafanua kuwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ilitumia kiasi cha shilingi milioni mia nne Hamsini na mbili laki moja thelathini na moja elfu mia tano Hamsini(452,131,550.00 ) ujenzi wa Barabara ya lami ya Mbwiga yenye urefu wa nusu kilomita(0.55km) mkandarasi akiwa kampuni ya WEBCO na Awamu ya pili Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kampuni ya Roadlight group limited zilisaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Mbwiga awamu ya pili kiwango cha lami yenye urefu wa nusu kilomita(0.5km) iliyopo Kata ya Isanga ikiwa na thamani ya shilingi milioni mia tatu sitini na saba laki sita ishirini na sita elfu mia mbili Hamsini (367,626.250.00) ambayo imeanza kutumika pamoja na miundombinu yake.

Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Jiji la Mbeya imekusudia kukusanya Mapato ya ndani shilingi Bilioni ishirini na mbili milioni mia tatu thelethini na tisa laki moja thelathini na moja elfu na mia tatu (22,339,131,300) na mapato ya ndani yasiyolindwa yanategemewa kutoa jumla ya shilingi Bilioni nane (8000,000,000) zitakazo tumika katika kujenga,kukarabati na kuboresha miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Kwa upande wa michezo baraza la madiwani kwa kushirikiana na watendaji kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuirejesha klabu ya Mbeya City kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kushuka Daraja misimu miwili iyoyopita,timu imepanda Daraja kwa kuweka rekodi tofauti tofauti ikiwa ni timu iliyopoteza michezo michache ambayo ni miwili tu,imekuwa klabu iliyoshinda michezo mingi nje ya nyumbani michezo 08                                                                | na kufunga magoli mengi kuliko timu zote za championship magoli 68

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AJIRA YA MKATABA KWA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU May 07, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO ( ORAL III C) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO (ORAL III B) April 23, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MAZUNGUMZO(ORAL III A) April 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI JIJI LA MBEYA LAJIVUNIA MIAKA 5 YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

    June 06, 2025
  • MAONESHO YA MBEYA CITY EXPO FURSA KWA WAFANYABIASHARA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA

    May 28, 2025
  • VIJANA MBEYA WAPIGWA MSASA WASISITIZWA KUZIFUATA FURSA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

    May 16, 2025
  • VIJANA MBEYA WAPIGWA MSASA WASISITIZWA KUZIFUATA FURSA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

    May 16, 2025
  • Tazama Zote

Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa

"MSITUBIPU KATIKA UCHAGUZI " RC MBEYA
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mbeya City Football Club
  • Google
  • Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ukurasa Maalumu

Tovuti Mashughuli

  • Poralg Website
  • Ikulu Website
  • Public Service Website
  • Tanzania Website
  • eGA
  • Secretariati ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea Tovuti

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    Mbalizi Road near TTCL Offices

    Anuani ya Posta: 149 Mbeya

    Simu: +25525252502372

    Simu ya Kiganjani: +255 25 2502563

    Barua Pepe: cd@mbeyacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbeya City Council . All rights reserved.